2014-04-09 08:02:45

Papa Francisko kuadhimisha Ibada ya Alhamisi kuu jioni na walemavu


Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu, Alhamisi kuu jioni, tarehe 17 Aprili 2014, kwenye Jumuiya ya Mfuko wa Don Gnochi, iliyoko mjini Roma. Siku ya Alhamisi kuu jioni, Mama Kanisa anaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kama sehemu ya kumbu kumbu endelevu ya Siku ile Yesu alipoweka Sakramenti ya Ekaristi Takatifu sanjari na Sakramenti ya Daraja Takatifu, zinazomwilishwa katika huduma ya upendo hasa kwa watu wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.

Jumuiya hii inawahudumia watu wenye matatizo ya afya wanaohitaji msaada wa pekee ili kuweza kurudia tena katika hali yao ya kawaida na kuingizwa tena katika maisha ya kijamii. Kimsingi ni watu wenye ulemavu, ambao wanapewa huduma kwenye Jumuiya hii ya Don Gnochi. Katika Ibada hiyo itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, wagonjwa, jamaa, wafanyakazi na uongozi wa kituoni hapo watashiriki.All the contents on this site are copyrighted ©.