2014-04-09 09:59:57

Mlipuko wa Ebola waitisha Guinea


Taifa la Guinea Afrika Magharibi linapambana na Changamoto ya virusi vya ebola, ambako mpaka sasa watu zaidi ya mia wamefariki dunia kwa virusi hivyo . Shirika la Afya la dunia limeeleza katika ripoti yake kwamba hii ni changamoto kubwa wanayopambana nao na inaweza ikawachukua kipindi cha miezi minne kuidhibiti.

WHO, inathibitisha kwamba watu 101 wamefariki Guinea na wengine 10 nchini Liberia kwa maradhi haya ambayo huua kati ya asilimia 25 hadi 90 kwa watu wanaoshikwa na virusi hivi vya ebola.

WHO inatahadharisha kwamba kipindi cha kati ya kuingiwa na mwanzo wa dalili, kinategemea hali ya afya ya mtu mwenyewe , baadhi huchukua muda mfupi kama siku mbili na wengine huchukua muda mrefu hata wiki tatu yaani siku 21. Hata hivyo , dalili za ugonjwa huu , kwa kawaida huanza siku minne hadi sita baada ya kuambukizwa ugonjwa huo. Dalili za kawaida ni kama: Kujisikia kuumwa na koo ,kuwa na homa, kikohozi kikavu cha kukatikakatika, udhaifu wa mwili , kuumwa vikali na kichwa, na misuli ya mwili, kuhara –kutoka mwa maji mwilini, pamoja na maumivu ya tumbo na kutapika.

Pia Upele, kwikwi, macho mekundu, na kutokwa na damu ndani na nje ya mwili, huonekana kwa baadhi ya wagonjwa. Rangi ya ngozi huvia na kuwa nyeusi , na mara nyingi upele hauonekani hadi hapo ngozi itakapoanza kuchunuka.

Kwa wanawake wajawazito, dalili za kawaida Ebola virusi huwa ni pamoja na kutokwa na damu nzito na mimba kutoka. Kifo kwa kawaida hutokea wakati wa wiki ya pili ya dalili. Waathirika kawaida wanakufa kutokana na kuwa na upungufu mkubwa wa damu.








All the contents on this site are copyrighted ©.