Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Fabio Fabene, Katibu mkuu msaidizi wa Sekretarieti
ya Sinodi za Maaskofu kuwa Askofu. Askofu mteule Fabio Fabene alizaliwa kunako tarehe
2 Machi 1959 mjini Roma. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 26 machi
1984 akapewa Daraja Takatifu la Upadre. Tangu wakati huo alipangiwa shughuli mbali
mbali katika maisha na utume wa Kanisa.
Tarehe Mosi, Januari 1998 akaanza utume
wake kwenye Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu na Mwaka 2010 akaendelea kuwa ni
Katibu mwambata Sekretarieti ya Baraza la Makardinali. Tarehe 8 Februari 2014, akateuliwa
na Papa Francisko kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu. Kitaaluma ni mwanasheria
na mwandishi mzuri wa vitabu.