2014-04-07 11:41:17

Benki ya Vatican kuendelea kutoa huduma kwa Kanisa Katoliki Ulimwenguni


Baba Mtakatifu Francisko amepitisha mapendekezo ya Benko ya Vatican, IOR, kwa siku za usoni kwa kutambua utume na dhamana yake kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa na Vatican katika ujumla wake. Mapendekezo haya yametolewa na tume na kamati mbali mbali zinazohusika na masuala ya fedha na uchumi mjini Vatican na kuwasilishwa kwa Baba Mtakatifu na Kardinali Santos Abril Y Castellò, Rais wa Tume ya Makardinali wa Benki ya Vatican, kama ilivyojadiliwa mwezi Februari 2014.

IOR itaendelea kutekeleza dhamana na wajibu wake kwa kutoa huduma za Kifedha kwa Kanisa Katoliki sanjari na kumsaidia Khalifa wa Mtakatifu Petro kutekeleza utume wake kama Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki, taasisi pamoja na watu binafsi wanaomsaidia Papa katika utekelezaji wa majukumu yake. Viongozi wakuu wa Benki ya Vatican wamepewa kazi ya kuhakikisha kwamba wanawasilisha mipango yao kwa Baba Mtakatifu, Baraza la Makardinali na Baraza la Kipapa la Uchumi.

Baba Mtakatifu pamoja na mambo mengine, anakazia umuhimu wa kuzingatia maadili ya kazi, ukweli na uwazi; kanuni na sheria zinazodhibiti masuala ya fedha mjini Vatican.All the contents on this site are copyrighted ©.