2014-04-05 13:56:02

Tembeeni na Neno la Mungu mifukoni mwenu!


Baba Mtakatifu Francisko kwa muda mrefu sasa ameendelea kuwahamasisha waamini kusoma, kulitafakari na hatimaye kulimwilisha Neno la Mungu kama dira na mwongozo wa maisha yao ya kila siku. Anawachangamotisha waamini walau kuwa na Biblia ndogo wanayoweza kuibeba mifukoni mwao, ili kufanya rejea kwa neno la Mungu katika hali mbali mbali za maisha kwa siku.

Ili kuyaweka mawazo haya katika matendo, Baba Mtakatifu, Jumapili tarehe 6 Aprili 2014 anatarajiwa kugawa Biblia kwa waamini na mahujaji watakaokuwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anakiri kwamba, katika Injili mwamini anaweza kumsikiliza Yesu anayeongea na wafuasi wake. Ni muhimu ikiwa kama mwamini atajiwekea utamaduni wa kutembea na kujisomea Neno la Mungu kila wakati anapopata fursa!







All the contents on this site are copyrighted ©.