(Vatican Radio) Mapema Jumamosi , 5 March, Baba Mtakatifu Francisko, alitembelewa
na Rais wa Liberia, Bibi Ellen Johnson Sirleaf. Baada ya kukutana na Papa , Rais Ellen
pia alikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin akiweko pia Askofu Mkuu
Domeniquè Mamberti, Katibu kwa ajili ya Mahusiano na nchi za nje Vatican.
Salaam
na majadiliano ya viongozi hao , vililenga zaidi uimarishaji wa mahusiano mazuri yaliyopo,
kati ya Jimbo la Papa na nchi ya Liberia , pande zote mbili zikionyesha kuridhika
na njia nzuri wanamotembea hasa katika mifumo ya kufanikisha demokrasia nchini Liberia.
Na kwa namna ya kipekee Rais Sirleaf, alisifu kazi za Kanisa katika ufanikishaji
wa amani na maridhiano ya kitaifa na kwa mchango wake mkubwa katika ustawi wa jamii,
elimu, demokrasia na maendeleo kwa ujumla. Na mwisho walizitazama kwa pamoja hali
halisi za kimataifa na kwa namna ya kipekee katika mkoa wa Afrika Kaskazini Magharibi
wakifanya rejea katika vipeo kadhaa vinavyoathiri eneo hilo.
Rais Ellen
Johnson Sirleaf, wa Liberia ni mwanamke wa kwanza Afrika, kuwa Mkuu wa nchi, na Mshindi
wa Tuzo ya Heshima ya Amani pia ni Mwenyekiti mwenza wa Jopo la ngazi ya juu la
watu mashuhuri linalo jadili agenda za Maendeleo baada ya kutimia kwa Malengo ya
milenia 2015 . Kwa sasa kuna andaliwa Malengo mengine yatakayo kuwa dira ya utendaji
katika kipindi cha miaka kumi na mitano ijayo.
Rais Sirleaf, katika mkutano
wake na waandishi wa habari, uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula
Duniani (WFP) siku ya Ijumaa, kwa lengo la kuzindua malengo ya ufanikishaji uhakika
wa chakula na lishe katika kaya, agenda za baada mwaka 2015, alisema, maelezo ya
Papa Francisko juu ya suala la umaskini ni makini na ya nguvu.
Na kwamba ,
maneno ya Baba Mtakatifu Francisko yataendelea kutoa mwangwi tena na tena, katika
mifano mingi, na inatoa msukumo wa nguvu, katika kushughulikia suala la umaskini
kama jambo muhimu kwenye agenda zote za maendeleo
Na kwamba, mashirika matatu
ya Umoja wa Mataifa WFP , IFAD na FAO alisisitiza, yanabaki kuwa vyombo vya lazima
vya kimataifa katika suala la kulisha dunia kama ni suala la kimataifa kwa ajili
ya uhakika wa chakula kufanikishwa. Akizungumzia suala hili la chakula katika nchi
yake mwenyewe, Rais alisema kuna hatua zilizopigwa ingawa juhudi zaidi bado zinahitajika.
Liberia
imeboresha uhakika wa chakula katika kiwango cha asilimia 43 kutoka asilimia 38. Rais
anatambua kiwango hicho bado ni cha chini, na hivyo watu wengi bado wanakabiliwa na
njaa hasa katika maeneo ya vijijini.
Rais Sirleaf pia ylionyesha haja
ya kutoa kipaumbele baada ya kutimia muda wa Malengo ya millenia yanayoishia 2015
kwamba, ajenda ya maendeleo ni si tu kupunguza umaskini lakini hasa ni kuelnga katika
kuutokomeza umaskini katika kila hali na aina ya mfumo wake. Na kumekuwa na makubaliano
ya jumla kwamba, ingawa masuala ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia yamekuwa na mafanikio
katika baadhi ya vipengere, bado kunahitajika kufanyika maboresho katika maisha
ya watu 840,000,000 waliobaki katika sugu njaa duniani.