Tafakari ya nne ya Padre Cantalamessa:imani katika Yesu Kristu, Mungu kweli na mtu
kweli
Wiki la nne la Mahubiri ya Kwaresima kwa Papa na Padre Cantalamessa “Imani katika
Yesu Kristo, Mungu kweli na mtu kweli”.
Padre Raniere Cantalamessa , Ijumaa
hii alitoa mahubiri ya nne ya kwaresima kwa Papa na wafanyakazi wa ofisi za Curia
ya Roma. Mahubiri hayo aliyagawa katika vipengere vinne: Kwanza amekizungumzia
kipengere kinacho unganisha Makanisa ya Magharibi na Mashariki, juu ya Yesu Kristo,
akisema ni muhimu kutambua kwamba kuna njia kadhaa zinazoelekea katika hatima moja
tu nayo ni Yesu Kristu. Baadhi wanapendelea kuchukua mbinu na njia za tangu mwanzo
wa Ukristu, yaani kusoma Bibilia. Pia , njia hiyo imegawanyika, kwa mara kadhaa kumfikia
Yesu, , kwa mfano. Kuna wale wanaoanza moja kwa moja kwa kusoma kitabu cha Biblia,
na kumfuata Yesu kwa namna yao, ambamo namo unaweza kufuata njia mbalimbali kwa
njia zilizotumiwa na wakongwe utoaji wa Katekesi juu ya yaliyoandikwa na kanisa ,
katika mwanga wa Neno na unabii wa Yesu tangu wakati wa Agano la kale , katika njia
yake ya kihistoria yenye kuhuisha maendeleo kumwamini imani, kwa kutazama tamaduni
mbalimbali za maisha ya mazingira yaliyoandikwa pia katika Agano Jipya. .
Padre
Cantalamessa anasema , Aidha Wakristu wanaoanza kwa kutafakari maisha ya watu na mahangaiko
na mateso yao , ya kila siku leo hii , akilinganisha na uzoefu wa maisha ya Yesu
na Biblia, katika kumgundua hasa Yesu yuko wapi. Ni kwa kumtambua yeye aliyofanywa
kuwa binadamu na kuja kukaa kati yetu ambaye amechukua juhudi za kutushindia dhambi
zetu , huyu ndiye Kristu, Mungu kweli na binadamu kweli katika nafsi moja.
2.
Padre Cantalamensa katika kipengere cha pili alizungumzia juu ya Yesu wa Kihistoria
na Kristu aliyaunganishwa tena katika mafundisho sadikifu ya Kanisa, akisema kwamba,
Ukweli halisi wa Yesu ulipita katika kipindi na majadiliano na ukosoaji mkali katika
karne mbili za mwanzo wa Ukristu ambamo mlikuwa na lengo la kuondoa yale yaliyofikiriwa
kuwa ni dhania tu za ugunduzi wa kiteolojia.
Lakini juu ya mada hii uliweza
kukamilika ka kuthibitisha mwendelezo kati ya Yesu wa Kihistoria Na Yesu anayetangazwa
daima, Bado tafiti zinazofanywa kuthibitisha mwendelezo kati ya Kristo wa kerygma
na Mafundisho ya Kanisa.
Padre Cantalamessa amehoji iwapo, utaratibu wa Mtakatifu
Leo Mkuu na Imani ya Kaldea, zinaweka alama ya maendeleo madhubuti ya imani kaiak
Agano Jipya au iwapo badala yake , inawasilisha utengano
Pia amezungumzia ziada
ya kuwa na kanuni akisema kwamba, kwa zaidi ya karne nne na nusu wanateolojia wamekuwa
wakifanya kazi ya ziada kutoa katika kanisa kanuni kwamba Yesu Kristo alikuwa ni Mungu
na Mtu mkweli. Au kwa kifupi alikuwa mtu mwenye kuwa na asili mbili. Na maandiko
yenyewe yanatuambia kuhusu nafasi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya ufahamu wa Yesu
kweli.