2014-04-03 15:26:36

Papa ahimiza Maaskofu wa Rwanda kuwa vyombo vya maridhiano.


Vatican Radio) Papa Francisko mapema Alhamis hii alikutana na mazungumza na kikundi cha Maaskofu wa Rwanda ambao wako katika hija ya kitume hapa vatican , “ad limina visit” . Katika hotuba yake iliyoandaliwa kwa ajili ya tukio hili, Baba Mtakatifu Francisko, alikumbua mauaji ya kimbari yaliyotokea 1994, miaka 20 iliyopita, akisema, kwa moyo wake wote, anaungana na Maaskofu na Wanyarwanda wote, katika kumbukumbu hii ya kusikitisha na kutisha. Na aliwahakikishia maombi na sala zake kwa ajili yao wenyewe , kwa jamii yao na kwa waathirika wote na familia zao, na anyarwanda wote , bila kujali dini , kabila siasa.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kwamba , miongo miwili baada ya matukio hayo kutisha , maridhiano na uponyaji wa majeraha y akiroho na ubinadamu, yanapaswa kubaki kipaumbele katika utume wote wa Kanisa, nchini Rwanda.

Na Hivyo aliwahimiza Maaskofu kudumisha dhamira yao na uwajibikaji katika juhudi za uponyaji na maridhiano ya kitaifa. Na kwamba, Msamaha wa dhambi na maridhiano ya kweli ,ni zawadi ya Kristo ambayo inawezekana kupokewa na kila binadamu, ata kama inaweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu kama jambo lisilo wezekana kutokana na mateso kama hayo waliyo yaishi watu wa Rwanda, katika kipindi hicho cha vurugu na mauaji ya kimbari. Papa ameonyesha kutambua kwamba, safari hii ya maridhiano kamili inaweza kuwa ndefu na yenye kuhitaji uvumilivu, mazungumzo na kuheshimiana. Papa Francis alisema , Kanisa katika nafasi yake , hivyo , linawajibika kutembea pamoja na watu hadi mwisho wa safari hii, kuwafariji na kuwapa matumaini bora kwenye njia hii ya mapatano ya kitaifa, kwa nguvu zao zote na katika imani yao na katika tumaini lote la Kikristo. Na aliiongeza kusonga mbele na hatua hii kwa kasi zaidi , hasa kwa njia za utoaji wa ushuhuda wa kweli mara kwa mara.

Wito kwa Maaskofu pia uliwataka Maaskofu kuonyesha mchango wa Kanisa kwa ajili ya manufaa ya wote, na kwa makini hususani katika mlengo wa elimu kama ufunguo Mkuu wa hali ya nchi kwa siku za baadaye. Papa Francis alisema, " Kwa hiyo ni wajibu wa Kanisa kuunda watoto na watu vijana, walio iva katika maadili ya Injili, na kuchota uzoefu hasa kwa neno la Mungu , ambalo ni dira inayoonyesha njia ya amani,mapatano na umoja..

Pia Papa Francis pia alizungumzia umuhimu wa jukumu la walei katika uinjilishaji na ujenzi wa mshikamano katika jamii , akisema kwamba, Maaskofu wanapaswa kutoa kipaumbele kwa mafunzo na msaada kwa watu wa kawaida, kwenye vyote, maisha ya kiroho na katika maisha ya kibinadamu na akili, na malezi bora.

Papa Francis alihitimisha kwa kuomba Msaada wa Mama Yetu ,Bikira Maria wa Kibeho, awaangazie wote. Upendo wa Maria kwa ajili ya watoto wake, hasa maskini zaidi na walio jeruhiwa kijamii, na kwa ajili ya Kanisa la Rwanda - na zaidi - kumgeukia kwa ujasiri, Mama yetu wa Huzuni ,ili kwa maombezi yake , Rwanda na dunia zima , ipate kupokea zawadi ya maridhiano na amani .










All the contents on this site are copyrighted ©.