Askofu mkuu Franco Coppola, Balozi Mpya wa Vatican Chad
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Franco Coppola kuwa Balozi Mpya wa Vatican
nchini Chad na ataendelea kuwa pia ni Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa
Afrika ya Kati. Haya ni maeneo ambayo yamekumbwa na vita pamoja na kinzani za kijamii.
Uteuzi huu unaonesha jinsi ambavyo Baba Mtakatifu Francisko anavyoguswa na mahangaiko
ya watu wanaoteseka kutokana na majanga mbali mbali ya maisha.