2014-04-02 15:10:36

Yatimia miaka tisa tangu kifo cha Yohane Paulo 11


(Vatican Radio ) Jumatano hii 02 Aprili, imetimia miaka tisa kamili tangu kilipotokea kifo cha Papa Yohana Paulo II, ambaye baadaye mwezi huu atatajwa Mtakatifu , pamoja na Papa Yohana XXIII.
Kardinali Leonardi Sandri , ambaye kwa wakati huu ni Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki , ambaye akiwa bado Askofu aliyefanya kazi kwa karibu sana na Yohana Paulo 11, ambaye miaka tisa iliyopita tarehe 2 Aprili alitangaza kifo cha Papa Yohana Paulo II, anasema hisia alizojisikia usiku ule wa kifo cha Yohana Paulo II, zilikuwa ni kubwa katika mwanga wa marehemu, kutajwa katika daraja la Watakatifu.
Kardinali Leonardo Sandri , anasema kwa sasa anazo hisia kwamba , hakustahili kwa wakati ule kufanya kazi na mtu huyu aliyekuwa mhubiri wa kweli na mtu wa amani , aliyeiishi imani yake kwa moyo mkuu na kwa unyenyekevu mkubwa katika huduma yake.
Katika mahojiano na Radio Vatican , Kardinali Sandri ameendelea kukumbuka ubinadamu wa kina wa Yohana Paulo II , akirejea uzoefu wake aliouona kwa Yohana Paulo II katika hali ya mateso ,dhuluma, hasara binafsi, na ujana wake na huduma katika nchi yake ya Poland yake ya asili na mazingira yaliyojenga uhasama na serikali ya nchi yake. “Ubinadamu wake, ulivishwa taji na Mungu na zawadi ya Roho Mtakatifu” alisema.
Yohana Paulo II , alikuwa na karama za kipekee katika kujenga urafiki na watu wa tamaduni mbalimbali na pia alikuwa na uwezo mkubwa katika masomo na haraka za kujua lugha mbalimbali duniani. Hata siku ya mwisho ya maisha yake alipokuwa taabani kitandani, ... alibaki mtupu hata katika mtazamo wa mali. Hapakuwa na aina yoyote ya anasa iliyomzunguka. Kardinali anasema, hivyo hatua Yohana Paulo II , kutajwa Mtakatifu , kwa hakika ni stahili yake yaliyojionyesha tangu wakati wa kifo chake.
Waamini waliokutana naye na walio fanya kazi naye , tangu awali waliamini kuwa ni mtakatifu tangu, kama ilivyosikika mara baada ya kifo chake kutangazwa, umati wa waamini ulipiga ukelele wa ' Santo subito ' katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , na sasa hakika kutoka kwa mamlaka ya Kanisa ... yanathibitisha mtu huyu ni Mtakatifu , yuko karibu kwa Mungu .... Yeye tayari anaonana na Bwana na hii ni linahakikishwa kwetu na Mkuu wa Kanisa , Baba Mtakatifu Francisko, wakati atakapoongoza Ibada kwa ajili ya kuwataja kuwa Watakatifu watumishi wawili wa Kanisa , Papa Yohana Paulo 11 na Papa Yohana XIII katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , 27 Aprili 2014.








All the contents on this site are copyrighted ©.