Ontario, Canada kumuenzi Yohane Paulo II kila mwaka
Baraza la Serikali ya Jimbo la Ontario Canada, limepitisha muswada wa sheria ambayo
imeanza kutumika kwamba, kila Mwaka ifikapo tarehe 2 Aprili, wataadhimisha Siku ya
Yohane Paulo II, kama kumbu kumbu endelevu ya kifo cha Papa Yohane Paulo II, kiongozi
wa Kanisa aliyesimama kidete kulinda na kutetea misingi ya haki, amani, upendo na
mshikamano wa kimataifa.
Hizi ni juhudi zilizofanywa na Mbunge Dipika Damerla
na muswada ukapita kwa kura za kishindo na tangu tarehe 17 Machi 2014, Sheria hii
imeanza kutumika na kwamba, tarehe 2 Aprili 2014 imekuwa ni siku ya kwanza tangu Sheria
hii ilipopitishwa.