2014-04-01 12:30:57

Wafundisheni na salini pamoja na watoto wenu!


Familia ya Kikristo ni mahali ambapo watoto wanapokea tangazo la kwanza la imani. Kwa sababu hii nyumba ya familia imeitwa kwa haki "Kanisa dogo la nyumbani", Jumuiya ya neema na sala, shule ya fadhila za kibinadamu na mapendo ya Kikristo.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa Familia za Kikristo katika maisha na utume wa Kanisa, leo katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawahimiza wazazi kuwafundisha watoto wao namna ya kusali vyema. Lakini pia anawataka kusali pamoja na watoto wao!







All the contents on this site are copyrighted ©.