2014-04-01 11:02:41

Rais Museveni ngangari!


Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Jumatatu tarehe 31 Machi 2014 amepokea maandamano makubwa ya wananchi wa Uganda wanaounga mkono ujasiri wake wa kupitisha muswada wa sheria unaopinga vitendo vya ushonga nchini Uganda.

Wananchi wa Uganda wanasema, Rais Museveni ameonesha ukomavu wa kisiasa, utu na maadili mema kadiri ya mila na mapokeo ya kiafrika na kamwe asikubali kuyumbishwa na propanda kutoka katika Nchi za Magharibi zinazotishia kusitisha, kufuta au kukata misaada ya maendeleo kwa Uganda. Viongozi wa dini mbali mbali nchini Uganda wamefanya Ibada ya pamoja kwa ajili ya kumwombea Rais Yoweri Kaguta Museveni katika utumishi wake kama Rais wa Uganda.

Akizungumza na wananchi wa Uganda, Rais Museveni anasema kwamba, Uganda haitishiki kwa nchi wahisani kutishia kusitisha misaada yenye masharti na inayochochea vitendo vya uvunjifu wa maadili na utu wema. Hadi sasa jumla ya dolla millioni 118 zimesitishwa kupelekwa Uganda, tangu Rais Museveni alipotia sahihi muswada wa sheria dhidi ya vitendo vya ushoga nchini Uganda.

Takwimu zinaonesha kwamba, Uganda ni kati ya nchi 37 kutoka Barani Afrika ambazo zinapiga rufuku ya vitendo vya ushoga. Rais Museveni anasema, ushoga hauna tija wala mashiko kwa wananchi wa Bara la Afrika. Tukio la kumshukuru Mungu kwa ajili ya ushupavu uliooneshwa na Rais Museveni limeandaliwa na Viongozi wa kidini nchini Uganda.







All the contents on this site are copyrighted ©.