2014-04-01 14:14:05

Papa na washauri wake wachambua Waraka wa Injili ya Furaha


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe Mosi, Aprili 2014 amekutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa Mabaraza, Halmashauri na Taasisi za Kipapa mjini Vatican. Agenda kubwa ya kikao hiki ilikuwa ni kufanya upembuzi yakinifu, tafakari na ushauri ulioibuliwa kutoka katika Mabaraza hayo kuhusu Waraka wa Kichungaji wa Baba Mtakatifu Francisko Evangelii Gaudium, Furaha ya Injili.

Katika mkutano huu, viongozi hawa wakuu wameangalia jinsi ambavyo Mama Kanisa anaweza kuumwilisha ujumbe huu katika maisha na utume wake. Mkutano huu ulianza hapo saa 3:30 asubuhi na kuhitimishwa saa 6:00 mchana kwa sala ya Malaika wa Bwana.







All the contents on this site are copyrighted ©.