2014-04-01 15:04:57

Maaskofu Katoliki wa Rwanda, wako Roma kwa hija ya kitume mjini Vatican


Maaskofu Katoliki wa Rwanda , wanatazamia kuwa na ziara yao rasmi ya Kitume ya siku moja, Alhamisi , 3 Aprili, 2014, kutembelea idara za Curia ya Roma na kukutana na Papa.
Asilimia 80 ya wakazi wa Rwanda wapatao milioni kumi ni Wakristu , ambao kati yao Wakatoliki ni karibia milioni tano.
Rais wa Baraza la Maaskofu kwa wakai huu ni Askofu Smaragde Mbonyintege , wa Jimbo la Kibgayi. Maaskofu wengine ni Askofu Mkuu Thaddée NTIHINYURWA, wa Jimbo Kuu la Kigali,
Askofu Philippe RUKAMBA wa Kitale,
Askofu Servilien Nzakamwita wa Byumba,
Askofu Jean Damascene BIMENYIMANA, wa Cyangugu
Jimbo la Gikongoro liko wazi
Askofu Antoine Kambanda wa Kibungo
Askofu Alexis HABIYAMBERE , S.J. wa Nyundo
Askofu Mkuu Vincent Harolimana wa Ruhengeri.







All the contents on this site are copyrighted ©.