Zaidi ya wananchi millioni moja kutoka Sudan ya Kusini, wanaoishi kwenye kambi za
wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum, wako hatarini kupoteza maisha yao kutokana
na baa la njaa na magonjwa ya mlipuko, ikiwa kama hali ya sasa haitafanyiwa maboresho
makubwa.
Sudan ya Kusini ambayo inakabiliwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe
inaweza kujikuta katika hali tete zaidi kutokana na mvua zinazoanza kunyeesha nchini
humo. Watoto, wanawake na wazee ndio watakaoathirika na hali hii ikiwa kama hakuna
hatua makini zitakazochukuliwa na Jumuiya ya Kimataifa.
Hayo yamebanishwa
na Bwana Yasmin Haque, mkurugenzi msaidizi wa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja
wa Mataifa, UNICEF, baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Sudan ya Kusini,
hivi karibuni.