Papa atahadhalisha: msiwe watalii katika safari ya imani
Papa Francisko , mapema Jumatatu hii, akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo
la Mtakatifu Marta alionya Mkristu kuwa na tabia ya kutangatanga kimaisha hasa maisha
ya kiroho. Alitoa wito kwa Wakristo wote kulenga moja kwa moja, katika kuzifuata
ahadi za Mungu, na kamwe kutokata tamaa.
Katika homilia hii amesema , kuna
Wakristo aminifu kwa ahadi za Mungu, katika maisha yao ya kila siku. Na pia kuna
wale wengine ambao imani yao kimaisha huyumbayumba, na bado kuna wengine wanao songa
mbele kwa kuifanya imani kama jambo la mpito.
Papa Francesco, ameelezea tofauti
zilizopo kati aina hizi tatu za waumini , akisema inasaidia kuelewa kwamba, maisha
ya Kikristo ni safari au hija ya kiroho. Papa alielezea kwa kurejea somo la kwanza,
lililosomwa kutoka Kitabu cha Isaya, akifafanua kwamba Mungu daima, hutimiza ahadi
zake, kabla ya mengine yote. Na ahadi yake ni uwepo wa maisha mapya, tena maisha
yenye furaha kamili ." Na kwamba, msingi mkuu katika hili ni fadhila ya matumaini
, na imani katika ahadi ya Mungu . Hiki ni kiini cha maisha ya kikristo. Papa amewataka
waamini wasikate tamaa kutembea katika njia hii ya imani licha ya magumu na changamoto
wanazoweza kupambana nazo.
Kwa bahati mbaya, aliendelea kueleza , kuna wale
wanaingia Ukristu, na baadaye huchoka na kujitoa. Wakristo hawa ni wengi! Wanakosa
matumaini na kukata tamaa. Wao wanaamini, kutakuwa na Mbinguni na yote yatakuwa
mazuri . Lakini wanashindwa kuifuta kwa uaminifu, njia inayoelekea katika ahadi hii.
Wao hukamilisha amri, maagizo na kila kitu , lakini wamesimama kando, na hivyo Bwana
hawezi kuwafanya kuwa chachu, kwa sababu wao hawatembei pamoja na Wakristo wengine
. Na hili ni tatizo. Na kuna wengine kati yao, ambao hukosea njia ,kama ilivyo kwetu
sote, na kutenda dhambi. kwa hawa tatizo hasa ni kule kutorudi katika njia, baada
ya kutambua kuwa wako nje ya njia, yaani kutotubu na kumrudia Bwana.
Papa
alieleza akilenga katiak somo la Injili, mbamo mtu mwenye imani anamwomba Yesu amponye
mtoto mgonjwa. Mtu huyo, alisadiki laichoambiwa na Bwana na kujiunga katika mwendo
wa kuelekea nyumba kwake bila wasiwasi wala mashaka na muda. alisubiri kwa imani
kwamba manae atapona. Papa amewaasa kwamba, Bwana anatuomba kama waamini sote tuungane
pamoja na kutembea katika njia moja ya kuuelekea Ufalme wake, Tusiipoteze njia kwa
kufuata njia zenye furaha za mpito katika maisha. Bwana anatutaka leo hii, tuyageuze
maisha yetu na kuzitazama ahadi za Bwana , kuwa watu wa Imani katika ahadi za Mungu.
Na kwamba Kwaresima ni wakati mzuri wa kufikiria kama tuko katika njia au
nje ya njia. Leo hii ni wakati wa kukata shauri na kujiunga katika barabara hii,
kusonga mbele na mwendo wa imani kwa ushupavu zaidi na zaidi, na si kuwa na teolojia
ya utalii, ya kuzunguka huko na kule, bila ya kusonga mbele kiimani.