Monsinyo Brian Ferme ateuliwa kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Brian Ferme kuwa Katibu wa Sekretarieti
ya uchumi iliyoanzishwa hivi karibuni mjini Vatican na Mwenyekiti wake ni Kardinali
George Pell na Mratibu mkuu ni Kardinali Reinhard Marx. Kazi kubwa itakayofanywa na
Monsinyo Brian Ferme ni kumsaidia Mratibu kutekeleza majukumu yake ya Baraza la Kipapa
la Uchumi ambalo limepewa dhamana ya kuratibu na kushughulikia masuala yote yanayohusu
utawala, fedha na uchumi mjini Vatican.
Monsinyo Ferme alizaliwa kunako mwaka
1955 ni Padre wa Jimbo Katoliki la Portsmouth,Uingereza. Alisoma falsafa, taalimungu
na sheria za Kanisa huko Melbourne, Oxford na Roma. Ni mwandishi maarufu wa vitabu
na mala kwenye majarida ya kimataifa. Amekuwa jaalimu wa Sheria za Kanisa Chuo Kikuu
cha Kipapa cha Gregorian na Laterano. Amekuwa ni “Dean of Studies” Kitivo cha Sheria
za Kanisa Chuo Kikuu cha Kikatoliki Marekani kunako mwaka 2003 na baadaye, alihamia
Venezia kuwa ni mkuu wa Kitivo cha Sheria za Kanisa cha Mtakatifu Pio wa kumi.
Kwa
miaka mingi Monsinyo Ferme amekuwa ni mjumbe wa Mabaraza kadhaa ya Kipapa mjini Vatican
hasa zaidi kama mshauri wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa pamoja na
Baraza la Kipapa la Sheria za Kanisa.