Kardinali Pietro Parolin, kuchangia utafutaji wa suluhu ya amani nchini Venezuela
Wananchi wa Venezuela wanaendelea kukabiliana na hali tete katika kipindi hiki cha
historia ya maisha ya nchi yao. Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican anasema,
Vatican inaendelea kufuatlia hali ya machafuko ya kisiasa nchini Venezuela na kwamba,
kuna uwezekano mkubwa kwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kutoa mchango
wake katika mchakato wa kutafuta suluhu ya machafuko ya kisiasa nchini Venezuela yanayoendelea
kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.
Kardinali Parolin anaifahamu
vyema Venezuela na anawapenda wananchi wake, anaendelea kufanya upembuzi yakinifu,
ili kuangalia jinsi gani Kanisa linaweza kuchangia katika upatikanaji wa suluhu ya
mgogoro wa machafuko ya kisiasa nchini Venezuela.