2014-03-29 11:54:48

Jimbo Katoliki la Cassano kutembelewa na Papa Francisko, hivi karibuni!


Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kutembelea Jimbo Katoliki la Cassano all'Jonio, lililoko Kusini mwa Italia na kwamba, taratibu na mipango inaendelea kufanyika mjini Vatican, ili kupanga tarehe maalum itakayomwezesha Baba Mtakatifu kutembelea Jimboni humo. Hayo yamesemwa na Askofu Nunzio Galantino, Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, mwishoni mwa Juma.

Anasema, Kardinali Angelo Bagnasco pamoja naye, walikutana hivi karibuni na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican na kuzungumzia kuhusu ziara hii ya kichungaji na kwamba, ameonesha utashi wa kutembelea Jimboni humo!







All the contents on this site are copyrighted ©.