2014-03-28 15:07:50

Tangazo Maalum la mabadiliko ya masafa.


Idhaa ya Kiswahili ya Redio Vatican inapenda kuwatangazia wasikilizaji wa Afrika Mashariki na Kati kwamba, tangu Jumapili 30 Machi 2014, kipindi kitasikika katika masafa tofauti na ilivyo sasa. Kipindi kitasikika katika masafa ya kHz 13765(21.799mb) au khz 15370 (19.51mb) muda ni uleule saa moja za jioni. Kipindi hicho kitasikika tena kesho yake katika ya Masafa mafupi ya Khz, 7360( mbd 40.76 )au kHz 9660 mb31.05 au kwa njia ya satelite, majira ya kumi na mbili na nusu za asubuhi (saa za Afrika Mashariki).

Kwa wasikizaji wetu wa Roma, tangu Jumapili kipindi kitasikika katika masafa ya FM 103.8, saa kumi na mbili kamili za jioni, na kitarudiwa kesho yake saa tatu na nusu za asubuhi katika masafa hayo hayo FM 103.8
Ukisoma tangazo hili, tafadhali mnong'onezee jirani yako. Tunaomba radhi kwa mabadiliko haya na kuwatakia usikilizaji mwema.








All the contents on this site are copyrighted ©.