Viwawa yahimiza vijana kuungana katika mapambano dhidi ya ukosefu wa ajira.
Vijana Wakristu wafanya kazi duniani kote wanahimizwa kujiunga katika vikundi mbalimbali
vya utendaji kwa ajili ya kupambana na ukosefu wa ajira, umaskini na utegemezi. Himizo
hilo limetolewa Alhamis hii na Monica Wanjiru, wa Kitengo cha Afrika katika Shirika
Katoliki la Kimataifa, kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za vijana Wakatoliki
duniani(VIWAWA) , lenye Makao yake Makuu hapa Roma. .
Monica Wanjiru ameeleza
juu ya juhudi hizi za Vijana Wakristu wafanya kazi(VIWAWA)kwamba ni mfumo unao unganisha
pamoja vijana, licha ya tofauti za hali, kazi na mazingira. Lengo Kuu la VIWAWA,
ikiwa ni kusaidia kuwaleta pamoja vijana, kutafakari na kuchukua hatua wenyewe ,na
kwa uhuru wao kamili, kukabiliana na yale yanayokuwa changamoto zinazo wazuia kuishi
maisha ya heshima na katika kutoa ushuhuda wao kwa uwepo wa Mungu katika Mpango wake
kupitia Yesu Kristo katika dunia ya kazi kwa vijana.
VIWAWA husaidiwa na Mapadre
na Masista na walei pia ,ambao huwasindikiza na kuwasaidia katika utume wao. Na kwamba
, utendaji huu wa pamoja licha ya kuwafanikisha vijana kuishi maisha ya kuheshimika
,pia husaidia kuona na kutoa msaada unahotajika kwa vijana wengine, kiroho na kihali
,na hivyo kufanikisha mabadiliko ya kimaisha, yaliyojengwa katika misingi ya upendo
na amani ya Mungu Mwenyezi kati yao.
Monica Wanijru, raia wa Kenya, ni kati
ya Waratibu wa shughuli za Vijana , katika Makao Makuu ya VIWAWA, yaliyopo hapa Roma.
Katika mahojiano na mahojiano na Redio Vatican, alielezea juu ya juhudi hizi, akianza
na kujitambulisha mwenyewe ..