2014-03-27 11:38:44

Padre Emmanuel Gihutu ateuliwa kuwa Gombera wa Seminari kuu ya "Saint Curè d'Ars" nchini Burundi


Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu amemteua Mheshimiwa Padre Emmanuel Gihutu kutoka Jimbo Katoliki la Ruyigi, kuwa Gombera wa Seminari kuu ya "Saint Curè d'Ars" iliyoko Jimbo kuu la Bujumbura, Burundi. Gombera mpya alizaliwa tarehe 25 Desemba 1959.

Kwa miaka mingi amekuwa akifanya utume wake kama Paroko na Mwalimu. Kuanzia Mwaka 1997 hadi Mwaka 2001 alijiendeleza kwa masomo ya juu huko Abijan. Aliporejea nchini Burundi alipangiwa kufundisha Falasafa kwenye Seminari kuu ya Jimbo kuu la Bujumbura na Burasira pia alikuwa ni Jalimu Butare, nchini Rwanda na Mratibu wa Chuo cha Makatekista, Jimbo Katoliki Muyange.

Kunako Mwaka 2010 alifaulu kupata shahada ya uzamivu katika falsafa, akateuliwa kuwa mkuu wa masomo na jaalimu katika Seminari kuu ya Bujumbura, Burundi na Chuo Kikuu cha Ziwa Tanganyika. Ni mwandishi wa vitabu kadhaa!







All the contents on this site are copyrighted ©.