2014-03-26 10:47:40

Marehemu Waziri mkuu mstaafu Adolfo Suarez Gonzales atakumbukwa na wengi!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambirambi kwa Askofu Jesus Garcia Burillo wa Jimbo Katoliki A'vila, Hispania kutokana na kifo cha Waziri mkuu mstaafu Adolfo Suarez Gonzales mwenye umri wa miaka themanini na moja, aliyefariki dunia hapo tarehe 23 Machi 2014 na kuzikwa tarehe 24 Machi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, katibu mkuu wa Vatican, anaiombea roho ya Marehemu Waziri mkuu mstaafu Suarez, pumziko la milele. Huyu ni kati ya viongozi mashuhuri nchini Hispania katika miaka ya hivi karibuni. Baba Mtakatifu anapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa wote walioguswa na msiba huu pamoja na kuwapatia baraka zake za kitume, akiwa na tumaini katika ufufuko wa wafu na uzima wa milele.







All the contents on this site are copyrighted ©.