2014-03-25 12:24:20

Monsinyo Marek Zalewski ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Zimbabwe na kupandishwa hadhi kuwa Askofu mkuu


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Marek Zalewski kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zimbabwe sanjari na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Marek Zalewski alizaliwa tarehe 2 Februari 1963 huko Augustow, Poland.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 27 Mei 1989. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Alianza kutoa huduma za kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 1995 na kupangia huko: Jamhuri ya Afrika ya kati, Umoja wa Mataifa, Uingereza, Ujerumani, Thailand, Singapore na Malaysia.







All the contents on this site are copyrighted ©.