Caritas inaendelea kuwasaidia waathirika wa vita nchini Mali
Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Italia, Caritas Italia, linaendelea kutoa msaada
wa hali na mali kwa waathirika wa vita iliyotokea nchini Mali kunako Mwaka 2012 hadi
Mwaka 2013. Hadi sasa bado kuna idadi kubwa ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi
wanaoendelea kupata msaada kutoka katika Mashirika ya misaada ya Kimataifa.
Hivi
karibuni, viongozi wa Kanisa nchini Mali waliomba msaada wa dharura kwa ajili ya kusaidia
kuwahudumia wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi wanaoendelea kuishi kambini. Mashirika
mbali mbali ya misaada ya Kanisa Katoliki yamekwisha kuchangia msaada kwa watu 65,
000. Caritas inatoa msaada pia Niger na Burkina Faso.