2014-03-21 15:24:47

Ukosefu wa ajira ni jeraha katika heshima ya utu wa mtu -Papa


(Vatican Radio) Baba Mtakatifu amewataka viongozi wote, wahakikisha heshima ya kazi na ajira inadumishwa kwa watu wote duniani, na hasa kwa nyakati hizi, dunia inapo pambana a changamoto ya ukosefu wa ajira. Aidha Papa amehimiza watu kuzama katika ubunifu mpya wa kazi, lakini wenye kuzingatia heshima ya utu wa mtu na mshikamano na umoja na wengine wote.
Papa aliyahimiza haya Alhamisi wakati akikutana na Wafanyakazi na viongozi wa Kampuni ya ufuaji vyuma ya "Terni" Italia ambayo ilikuwa ikiadhimisha miaka 130 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Papa Francisko alikutana na wafanyakazi hao katika ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican. Mkutano huu ulifanyika kwa uvuvio wa Roho ya kufanya upya uwepo wa karibu wa Kanisa katika dunia ya kazi, kama inavyohamasishwa na Papa Francisko. Wito wa Papa unahimiza kwa nguvu , waajiri wote kutoa kazi za heshima kwa waajiri wote. Na kwa ajili ya kukishinda kipeo cha ukosefu wa ajira, alisisitiza haja ya kuwa watu wabunifu na wakti huohuo kujenga mshikamano na umoja wa kushirikishana matunda ya kazi zinazopatikana, kwa haki.

Mkutano huu wa Wafanyakazi wa Terni na Papa Francisco, ni juhudi za Mtawala wa Kitume wa Terni –Narni Amelia , Mons. Ernesti Vecchi, amba ye katika mahojiano na Redio Vatican amesema , mbele ya hali halisi za na mgogoro wa sasa wa kiuchumi, ni muhimu kuthibitisha tena kwamba, kweli kazi ni muhimu kwa jamii, familia na watu binafsi , kama alivyo sisitiza Papa Francisko kwa nguvu, katika hotuba yake kwa wafanyakazi hao wa “Terni steelworks” na familia zao, kwamba kazi inahusiana moja kwa moja na maisha ya mtu, ikiwa ni pamoja na uhuru wake na furaha zake.

Na kwamba, Thamani msingi ya kazi ni heshima yake kwa binadamu, kwa sababu hufanikisha matazamio ya mtu na uwezo wake wa akili, ubunifu na utendaji. Kutokana na hili kinachofuata ni kwamba kazi si tu faida za kiuchumi , lakini pia, zaidi ya yote, ni hatima yake katika kutimiza mapenzi ya mtu na kulinda heshima ya utu wake. Na hivyo, hadhi ya binadamu, hushikamana daima na kazi ," aliongeza Papa na kuunga mkono ujumbe uliotolewa na watu kadhaa waliokosa ajira.

Watu hao walitoa malalamiko yao kwa Papa, baadhi yao wakiwa wafanyakazi vijana ambao wamepoteza kazi, ambao walieleza hali zao halisi kwamba, wana familia, na hivyo wanaendelea kuwa Baba wa mji, lakini asiyekuwa hata na uwezo wa kumlisha mkewe na watoto, na hivyo wanabaki kutegemea chakula cha msaada kila siku , au kutoka Parokiani au katika mashirika ya misaada ya kibinadamu kama Chama cha Msalaba Mwekundu , au Caritas. Baba, hao wamweleza Papa Francisko jinsi wanavyojisikia utu wao kudhalilika kwa kukosa kutimiza wajibu wao msingi wa kuleta mkate nyumbani , kwa sababu hawana jinsi ya kuupata mkate huo bila ya kuwa na kazi. Na inakuwa kama hakuna kazi pia heshima na utu wa mtu
Papa Francisko katika maelezo yake alitafakari tatizo hili kubwa la ukosefu wa ajira ambalo sasa lina athiri idadi kubwa ya wakazi wa nchi za Ulaya, akisema ni matokeo ya mfumo wa uchumi ambao hauna tena uwezo wa kujenga ajira mpya za kazi kwa sababu mfumo huo umeweka kitu kiitwacho fedha kuwa kama muungu wake, mwenye kupendelea moyo wa ubinafsi, majivuno na choyo cha kujilimbikizia bila kujali wengine. Kwa hiyo, inakuwa ni jambo muhimu kwa mifumo mbalimbali ya kisiasa , kijamii na kiuchumi, kukuza mbinu mbalimbali za kufanikisha ajira lakini kwa kuzingatia haki, umoja na mshikamano na wafanyakazi wote, ili kwamba kinachopatikana ni kw amanufaa ya jamii nzima.

Ubunifu wa wajasiriamali na mafundi jasiri, kutazama mbele, siku zijazo kwa ujasiri na matumaini. Na mshikamano miongoni mwa jamii nzima, kutokata tama , lakini pia kusonga mbele na maisha kwa akili zaidi na mshikamano na wali ambao wako katika hali mbaya za kupungukiwa. Na hii ni changamoto , kwa jumuiya nzima ya Kikristo. Papa aliwa hakikishia ukaribu wake na kuomba maombezi ya Kimama ya Bikira Maria juu ya sasa na jimbo zima la Terni , " hasa ulimwengu wa kazi, familia zilizo katika shida na hatari ya kupoteza utu wao, kwamba hawana kazi , na pia kwa ajili ya watoto na vijana na wazee wao.








All the contents on this site are copyrighted ©.