Padre Cantalamessa : Tafakari ya Pili kwa Papa na Wasaidizi wake wa karibu katika
Idara za Curia.
(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko na wasaidizi wake katika ofisi za Curia
ya Roma, mapema ijumaa hii, walikuwa na kipindi cha ukimya cha kusikiliza tafakari
ya neno la Mungu kutoka kwa Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri katika Makazi ya Kipapa
kwa wakati wa Kwaresima. Ijumaa hii ametoa tafakari yake ya pili kwenye mfululizo
wa tafakari za Siku za Ijumaa, katika kipindi cha Kwaresima.
Tafakari ya Padre
Cantalamessa , ililenga zaidi kwa Mtakatifu Agustino, chini ya Mada " Nasadiki
Kanisa ni Moja Takatifu. Hotuba yake aliigawa chini ya vipengere vinne,1. Kuhama
kutoka kanisa la Mashariki hadi Magharibi, 2. Kanisa ni nini 3. Ufunuo wa kikanisa
wa Mtakatifu Agustine leo hii una maana gani . 4 Msharika wa Mwili wa Kristo, aliyehasishwa
kwa Roho mtakatifu.
Katika maelezo yake, Padre Cantalamessa alirejea utangulizi
wa tafakari ya wiki iliyopita ambamo walitafakari maana ya kipindi hiki cha kwaresima
kwamba, ni wakati wa kwenda jangwani na Yesu, kufunga na vyakula na maonyesho ya
picha zinazo onyeshwa katika runinga na vyombo vingine vya habari , na hivyo kujifunza
kushinda majaribu, na juu ya yote, kukua katika kujenga uhusiano wa karibu na Mungu.
Na
ameeleza kwamba katika mahubiri manne yaliyo salia, ataendelea kutafakari juu ya
mada aliyoianza katika Kwaresima ya 2012 juu ya Mababa wa walimu wa Kanisa , na baada
ya Mababa wa Kanisa la Kigriki kwa sasa anatazama kwa makini maelekezo yaliyotolewa
na Mababa wa Kanisa waliofuatia , Mtakatifu Augustine, Mt. Ambrose , Mt. Leo Mkuu,
Mt. Gregory Mkuu, kwa ajili ya kuona , nini kila mmoja wao anasema kwetu leo hii,
kuhusu ukweli wa imani. Na kwa mtiririko huo, asili ya kanisa , uwepo halisi wa
Kristo katika Ekaristi, Mafundisho ya Kanisa ya Kaldonia, na ufahamu wa kiroho wa
maandiko.
Padre Cantalamessa anataja lengo la utajiri uliomo katika mafundisho
ya walimu hawa wakuu wa kanisa, kuwa ni kuthibitisha uzuri na furaha ya kuamini
, kama anavyosema Mtakatifu Paulo, kwa maana haki ya Mungu itadhihirisha ndani yake
toka imani hata imani " (Rom 1:17), toka imani hata akili na moyo, na Mwenye Haki
ataishi kwa imani. Inakuwa ni kuongeza kiwango cha imani ndani ya kanisa na hivyo
kuwa chemichemi ya kutangaza neno la Mungu limwenguni kote.
Padre Cantalemessa
aliendelea kuzungumzia mafundisho mbalimbali ya Mababa wa Kanisa , tangu nyakati za
mwanzo wa kanisa katika mitazamo mbalimbali ya Utakatifu wa Kristo ,Roho Mtakatifu
na Utatu Mtakatifu , na katika kumjua Mungu , kwamba mtu anaweza kuwa na hisia kwamba
kulikuwa na mambo machache sana yaliyo bakia kwa Mababa wa Kanisa kufanya mabadiliko
katika mafundisho sadikifu kwa Wakristo. Na kwamba, wakiwa wamehamasika kwamba wao
ni sehemu ya utamaduni huo wa Kikristo, walikuwa na wajibu mkubwa katika kutoa maelekezo
sahihi kwa Kanisa, wakichochewa na barua za Mtume Paulo , kutafakari juu ya mandhari
ya neema , Kanisa , sakramenti, na maandiko Matakatifu .
Na akirejea ufunuo
wa Mtakatifu Augustine kwa kanisa leo hii anasema , kuna mabadiliko makubwa duniani
na katika kanisa na hata kiteolojia tangu wakati ule wa Mtakatifu Agustine. Na hivyo
kwa Mkristo ni suala la kuanza kutazama upya na kwa unyenyekevu wa nyakati , kwa ajili
ya kuugundua upya yalifumbatwa katika utu wa Kristo. Tunahitaji kujiweka katika wakati
ule wa Mitume , waliopambana na ulimwengu wa kipagani, kama ilivyo kwa wakati huu
Kanisa linakabiliana na watu wakristu walioasi.
Mtume Paulo kwa maneno mafupi
alisema, kazi ya thamani ya Mkristo ni kuitangaza Injili ya Kristu aliyesulubiwa
na kufufuka. Na hii haina maana kwamba ni kupunguza ukuu wa teolojia na utajiri wa
kiroho unaotokana na marekebisho yanayofanyika au kurudi katika taratibu na kanuni
za awali , bali kama njia ya kuruhusu Ukristu kuwaleta watu wengi zaidi ndani ya kanisa
ambalo ni Mwili wa Kristo mwenyewe.