Jumanne jioni, katika Kanisa dogo la Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbanian, Roma, Kardinali
Fernando Filoni, Mkuu wa Decania ya Makardinali, aliongoza Ibada ya Misa, kwa nia
ya kumtolea Mungu shukurani, kwa Kardinali Josef Tomko , kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa.
Katika kanisa hilo Kardinali Tomko amefanya Ibada ya aina hii ya kusherehekea Siku
Kuu ya Kuzaliwa kwa mara 16.
Shirika la habari la Fides , limetaarifu kwamba,
Kardinali Josef Tomko aliisherehekea miaka yake 90 ya kuzaliwa, akiwa amezungukwa
na mrithi wake katika huduma ya Umisionari, Kardinali Fernando Filoni, na Makardinali
wengine akiwemo Kardinali Angelo Sodano, Maaskofu wakuu na Maaskofu, Mapadre , Watawa
na marafiki zake wenye wanaoendelea kuwa nae karibu katika utumishi wake kwa muda
mrefu kwa Kanisa. Aidha, walikuwepo wafanyakazi wa Usharika kwa ajili ya Uinjilishaji
wa Watu , Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Misioni, pamoja na wengine wengi.
Kardinali
Filoni , katika homilia yake alitoa shukurani zake za dhati kwa Kardinali Tomko, kwa
yale aliyoyafanya na yale ambayo bado anatarajia kuyafanya kwa ajili ya kujenga umoja
kamili wa kanisa na kwa mchango wake hususani katika kazi za kimisionari .
Amesema,
tunamshukuru kwa ajili ya mbegu nzuri aliyoipanda katika Kanisa, na kwa ushuhuda
wake katika maisha ya kipadre, na hivyo wakati wa sherehe hii, kwao unakuwa ni wakati
muafaka wa kutafakari nini maana ya maisha ya Kardinali Tomko katika kanisa na jamii
kwa ujumla. Kardinali Tomko alizaliwa( Machi 11 1924) na alipadirishwa ( Machi 12,
1949 ), kufanywa Askofu ( Septemba 15, 1979 ). Hivyo ametimiza miaka 65 ya upadre
na miaka 35 ya kuwa Askofu. Kardinali Filoni, aliendelea kutoa wasifu mfupi wa
Kardinali Tomko kwamba , katika miaka yake tisini ,akiwa mzaliwa wa tafa lake pendwa
la Slovakia, kwamba katika miaka ya ’40, alikamilisha masomo yake katika Chuo Kikuu
cha Gregorian na Lateran ambako alijipatia shahada katika Teologia, sheria za kanisa,
na Sayansi ya jamii. Wakati huo taifa lake lilikuwa katika giza nene la Ukomunisti
na Slovakia ikiwa chini ya himaya Urusi. Na kwa miaka miaka 15 yalikuwa ni makamu
wa gombera wa Chuo cha Kipapa Nepomuceno , kabla ya kuwa Chini ya Usharika kwa ajili
ya Maaskofu , na kisha, tangu mwaka 1979 , alifanywa kuwa Katibu Mkuu wa Sinodi ya
Maaskofu. Na alitajwa kuwa Askofu na Mwenyeheri Yohana Paulo II tarehe 15 Septemba
1979. Baada ya miaka 6 , Aprili 24, 1985 aliteuliwa na Papa kuwa Mkuu wa Usharika
kwa Uinjilishaji wa Watu , na wakati huo huo, Kansela wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana.
Katika mwaka huo huo , Mei 25, 1985, akawa Kardinali Shemasi.
Kadi. Filoni
alieleza katika miaka yake 16 ya kuliongoza Shirika kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu,
aliweza kufunga safari nyingi katika utume wa kimisionari, na alitoa msukumo mkubwa
kwa maisha ya utume wa kimisionari hasa uimarishaji wa Makanisa vijana na majimbo
mengi ya Afrika, Asia, Oceania na Amerika.