2014-03-19 10:14:16

Upendo wa Kikristo hauna mipaka!


Kati ya mambo yanayoendelea kupewa kipaumbele cha pekee na Baba Mtakatifu Francisko ni upendo kwa Mungu na jirani; umuhimu wa kuchuchumilia huruma ya Mungu kama njia ya kujitakasa na kuyatakatifuza malimwengu. Maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii kutokana na umaskini wa: hali na kipato; maadili na maisha ya kiroho, waonjeshwe upendo wa Mungu usiokuwa na mipaka kwa waja wake.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, upendo wa Kikristo hauna mipaka. Haya ndiyo mafundisho yanayotolewa na Yesu Kristo, kielelezo cha Msamaria mwema.







All the contents on this site are copyrighted ©.