Tamko la Maaskofu lasema: Papa Francisko hatatembelea Uganda mwaka huu.
Askofu Mkuu John Baptist Odama wa Jimbo Kuu la Gulu na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Uganda,kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda , anawafahamisha Wakristu
wote wa Uganda na dunia kwa ujumla kwamba, Papa Francisko, pamoja na kupokea kwa
moyo mkunjufu mwaliko wa kuitembelea Uganda wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka
hamisini tangu wafia dini wa Uganda kutangazwa kuwa Watakatifu,kutokana na msongamano
wa shughuli zingine zilizokuwa zimeandaliwa awali, kwa mwaka huu hataweza kwenda
Uganda kuongoza sherehe za Jubilee hiyo, iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 18 Oktoba
2014. .
Taarifa inabaini, Septemba 2013, Maaskofu Katoliki wa Uganda walituma
mwaliko wao kwa Papa Francisko wakimwoba aitembelea Uganda, kuhitimisha Maadhmisho
ya Jubilee ya kutimia miaka 50 tangu wafia dini wa Uganda kutangazwa Watakatifu.
Baada
ya kupata jibu la mwaliko wao, Maaskofu ya tarehe 14 March 2014,waliandika barua kuwafahamisha
waamini kwamba, Papa Francisko hataweza kwenda Uganda mwaka huu, kutokana na ratiba
yake kuwa nzito. Na hivyo wameamua kuahirisha maadhimisho ya sherehe hizo kitaifa
hadi hapo maelekezo mengine yatakapotolewa. Na hivyo kwa matumaini wanasali ili
ratiba ya Papa, ipate hata mwanya mdogo wa kumruhusu kuitembelea Uganda, katika siku
za hivi karibuni.
Pia Maaskofu katika barua yao, wametangaza kwamba, Siku Kuu
ya Wafia Dini wa Uganda ambayo huadhimishwa tarehe 3 June itafanyika kama kawaida
chini ya usimamizi wa Jimbo la Kotido.
Maaskofu wanawatakia waamini wote, utajri
wa kiroho katika kipindi hiki cha kwaresima na baraka nyingi za Mungu.