Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, Mwenge wa Amani alioubariki baada
ya Katekesi yake kwa Siku ya Jumatano tarehe 19 Machi 2014, utasaidia kuhamasisha
upatikanaji wa amani ndani ya mioyo ya watu. Mwenge wa Amani ulipelekwa na wajumbe
kutoka Shirika la Wabenediktini waliosindikizwa na waamini kutoka Norcia, Subiaco
na Casino, nchini Italia.
Mwenge wa Amani utaanza kutembezwa kwenye baadhi
ya Monasteri za Wabenediktini na baadaye utarudishwa kwenye miguu ya sanamu ya Mtakatifu
Benedikto.