2014-03-17 08:39:03

Siku kuu ya Mtakatifu Patrick, iwe ni siku ya kuonesha mshikamano na watu wanaoteseka!


Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland, linawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema, katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Mtakatifu Patrick, Msimamizi wa Ireland, kusali kwa ajili ya kuombea imani thabiti na ustawi wa wananchi wa Ireland katika ujumla wao.

Wananchi wanaadhimisha Siku kuu hii Jumatatu tarehe 17 Machi 2014, wakati ambapo familia nyingi zinaendelea kuteseka kutokana na athari za myumbo wa uchumi kimataifa, hali ambayo imepelekea familia nyingi kutengana, kutokana na ukosefu wa fursa za ajira. Ni siku maalum kwa ajili ya kuwaombea na kuwashirikisha wageni na wahamiaji katika maisha yao kwa kutambua kwamba, hata Mtakatifu Patrick, alikuwa mhamiaji, aliyeonja ukarimu na upendo kutoka kwa jirani zake.








All the contents on this site are copyrighted ©.