Ili wote wawe wamoja ndiyo kauli mbiu itakayoongoza hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu
Francisko katika Nchi Takatifu kuanzia tarehe 24 hadi 26 Mei, 2014, kama sehemu ya
kumbu kumbu ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana, kusali na kuzungumza
na Patriaki Anathergoras mjini Yerusalemu.
Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa
anatangaza hija hii alisema kwamba, hii ni hija ya sala itakayomwezesha kutembelea
Yordan, Palestina na Israeli. Maeneo yaliyolengwa ni Amman, Bethlehemu na Yerusalem.
Akiwa mjini Yersalemu, Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki Bartolomeo wa kwanza pamoja
na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo nchi Takatifu watasali kwenye Kaburi Takatifu,
ili kuombea umoja wa Kanisa. "Utu unum sint" Ndiyo Kauli mbiu inayoongoza hija ya
Baba Mtakatifu Francisko huko katika Nchi Takatifu.
Itakumbukwa kwamba, Baba
Mtakatifu Francisko anakuwa ni Papa wa tatu kutembelea na kusali katika Nchi Takatifu.
Wengine ni: Papa Paulo VI aliyetembelea Nchi Takatifu kuanzia tarehe 4- 6 Januari
1964. Mwenyeheri Yohane Paulo II alitembelea huko kuanzia tarehe 20- 26 Machi 2000. Papa
mstaafu Benedikto XVI alifanya hija ya kichungaji kuanzia tarehe 8 hadi 15 Mei 2009