2014-03-14 08:27:58

Salam za rambi rambi kutokana na kifo cha Kardinali Josè da Cruz Polycarpo


Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa majonzi na huzuni kubwa habari za kifo cha Kardinali Josè da Cruz Policarpo aliyefariki dunia Jumatano tarehe 12 Machi 2014, akiwa na umri wa miaka 78. Baba Mtakatifu anaungana na wote walioguswa na msiba huu kwa njia ya sala.

Baba Mtakatifu anapenda kumweka marehemu Kardinali Policarpo chini ya tunza na huruma ya Mungu, akikumbuka mchango wake katika ustawi na maendeleo ya Kanisa. Ni Mchungaji aliyejikita katika kutafuta ukweli, akajitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya kuwaongoza Maaskofu wenzake kama Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ureno.

Ni Kiongozi aliyejitahidi kuwatangazia Watu wa Mungu Injili na atakumbukwa sana kutokana na mchango wake kwenye Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ureno. Baba Mtakatifu Francisko anamweka Marehemu Kardinali Polycarpo chini ya maombezi ya Bikira Maria.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican naye pia ametuma salam za rambi rambi kutokana na kifo cha Kardinali Polycarpo. Jimbo kuu la Lisbon, Ijumaa jioni linaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumwombea Marehemu Kardinali Polycarpo inatarajiwa kuomngozwa na Patriaki Manuel Josè Macario do Nascimento Clemente wa Jimbo kuu la Lisbon na baadaye atazikwa kwenye makaburi ya Mapatriaki wa Lisbon.







All the contents on this site are copyrighted ©.