2014-03-13 12:05:16

Mheshimiwa Padre Antoine Sabi Bio ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Natitingou, Benin


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Antoine Sabi Bio, aliyekuwa Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Natitingou kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Natitingou, nchini Benin. Askofu mteule alizaliwa kunako mwaka 1963.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 7 Desemba 1991 baada ya hapo akaendelea na masomo ya juu Chuo Kikuu cha Wasalesiani wa Don Bosco, Roma na kuhitimu masomo yake tarehe 19 Juni 2002. Tangu wakati huo amepangiwa majukumu mbali mbali kama Msarifu wa Jimbo, Paroko, Gombera na Makamu Askofu.

Tangu Mwaka 2009 hadi mwaka 2013 Alikuwa Paroko. Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa ni Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki Natitingou, Benin,, utume ambao ameuendeleza hadi kuteuliwa kwake kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo la Natitingou, Benin.







All the contents on this site are copyrighted ©.