2014-03-12 11:29:33

Onesho la Picha za hija ya Papa Paulo VI mjini Yerusalemu


Viongozi wa Makanisa ya Kikristo mjini Yerusalemu wamefungua onesho la picha kati ya Patriaki Anathegoras wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli na Papa Paulo VI walipokutana, wakasali na kuzungumza pamoja, miaka 50 iliyopita. Hizi ni picha zinazonesha hotuba na zawadi zilizotolewa na Papa Paulo VI alipotembelea Nchi Takatifu.

Haya yote ni maandalizi ya hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Nchi Takatifu atakaoifanya mwishoni mwa Mwezi Mei, 2014, kama sehemu ya Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na kuzungumza na Patriaki Anathegoras wa Costantinopoli, katika harakati za kujenga na kudumisha majadiliano ya Kiekumene miongoni mwa Wakristo.







All the contents on this site are copyrighted ©.