2014-03-07 11:29:03

Ujumbe wa Papa kwa wajumbe wa Baraza la Kiekumeni la Makanisa.


Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa wajumbe wa Baraza la Kiekumeni la Makanisa, ambao wako Roma kwa lengo la kukutana na Baraza la KIpapa kwa ajili ya Umoja wa Wakristo, umetaja mkutano huo kuwa ni alama zaidi ya hatua mbele na muhimu katika mahusiano ya muda mrefu na matunda kati ya Kanisa Katoliki na Baraza la Makanisa Duniani. Na kwamba askofu wa Roma anaonea fahari na kutoa shukurani kwa kazi wanayo ifanya kwa msaada wa umoja wa Wakristo.

Katika ujumbe huo, Papa ametambua kwamba, tangu kuanzishwa kwake , Baraza la Makanisa ya Dunia, limechangia kwa kiasi kikubwa na kufanya Wakristo wote kufahamu kwamba mgawanyiko wa Wakristu, ni kikwazo kikubwa katika kuwa mashahidi wa Injili duniani. Na hivyo Papa anaasa, si vyema kwa Wakristu kuendelea na mgawanyiko huu, kama vile hawana uzoefu wa kihistoria wa Kanisa, unao weza kuepusha kipingamizi hicho. Na kwamba iwapo Wakristo watapuuza wito wa umoja ,unaotoka kwa Bwana , wanajiweka katika hatari ya kumpuuza Bwana mwenyewe na wokovu tunaoupokea kupitia sadaka ya mwili wake Kanisa. Hakuna sehemu nyingine ya wokovu, wala jina jingine linalo weza kutuokoa. ( Matendo 4:12).

Papa ameendelea kukiri kwamba, Uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na Baraza la Makanisa, ulio anzishwa tangu Mtaguso Mkuu wa Pili , unaendelea kufanikisha kwa dhati ushirikiano wa kiekumeni na kutia nguvu zaidi katika juhudi za kuwasiliana na kubadilishana zawadi za uzoefu kati ya jumuiya na hivyo kuvishinda vishawishi vya kutoelewana pande zote. Hata hivyo , njia ya kufikia umoja kamili bado ni njia ndefu na ngumu. Lakini Roho Mtakatifu anaendelea kuwatia nguvu na kuwahijmiza wote kutoogopa kuupanda mlima wa ushirika kamili, kutoogopa kuridhika na maendeleo yaliyofikiwa miaka ya hivi karibuni, na kusonga mbele kwa uaminifu.

Na kwamba, Maombi ni ya msingi wa safari hii. "Ni kwa roho tu ya unyenyekevu na sala isiyokoma , tutaweza kuwa na uwezo wa kuona muhimu kusonga mbele kwa utambuzi na motisha kutumikia familia ya binadamu katika mapambano yake yote na mahitaji yote ya kiroho na kimwili".

Papa amekamilisha ujumbe wake kwa kuwahakikishia maombi yake wakati mkutano wao na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo, unaofanyika kwa lengo la kupiga hatua mbele katika njia hii ya imani kwa pamoja. Amesema, “Roho wa Bwana na amdumishe kila mmoja wenu na familia zenu, wenzenu wote katika Baraza la Makanisa la Dunia na wote wenye kuwa na hamu ya kujenga umoja huu wa Wakristu kwa moyo wa dhati. Niombeeni nami pia, ili Bwana aweze niruhusu kuwa chombo cha utulivu katika kuyatimiza mapenzi yake na kuwa mtumishi wa umoja . Amani na neema ya Bwana iongozane nanyi nyote”.








All the contents on this site are copyrighted ©.