Rufuku ya biashara ya silaha bado ipo nchini Somalia
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio linalopiga
rufuku biashara ya silaha ndogo ndogo nchini Somalia hadi kufikia tarehe 25 Oktoba
2014. Rufuku ya Umoja wa Mataifa dhidi ya silaha kubwa na nzito itaendelea kufanyiwa
kazi na kwamba, Serikali ya Somalia inawajibu wa kimaadili kuhakikisha kwamba, azimio
hili linatekelezwa kikamilifu.
Serikali ya Somalia ilikuwa imeliomba Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa rufuku ya biashara ya silaha ili kuiwezesha
Somalia kujizatiti katika masuala ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao dhidi
ya vitendo vya kigaidi nchini humo.