2014-03-07 09:06:30

Papa Francisko: hakuna mtindo wa maisha ya Kikristo" bila Yesu au Msalaba


(Vatican Radio) Unyenyekevu, upole, ukarimu ni “mtindo” katika njia ya maisha ya Mkristo, ni njia ya maisha inayoelekea katika njia Msalaba, kama Yesu alivyofanya, na ni maisha yanayoongoza katika furaha . Huo ilikuwa ni ujumbe wa Papa Francis katika hotuba yake juu ya Alhamisi wakati wa Ibada ya Misa katika Kanisa ndogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican.

Mafundisho ya Papa yaliilenga Injili ya Alhamisi baada ya Jumatano ya Majivu , ambamo Yesu anawaambia wanafunzi wake : "Kama mtu yeyote anataka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe na achukue msalaba wake kila siku, anifuate” . Huo ndiyo mtindo wa maisha ya Mkristu , Papa alisisitiza, ndiyo mtindo wa maisha kwa sababu, uliwekwa na Yesu mwenyewe, kwa mara ya kwanza katika vitendo.
Na hivyo inakuwa ni vigumu kuyafikiria maisha ya Mkristo nje ya njia hii . Daima ni safari na ni njia aliyoichagua yeye kwanza kwa unyenyekevu, na upole, kujitolea sadaka na hatimaye kupanda. Na hivyo katika njia hii , pasipo Msalaba, mtindo wa maisha ya Mkristo, yanakuwa si ya Mkristo , na Msalaba bila Yesu, huo si msalaba wa Kikristo. Mtindo wa maisha ya Mkristo ni kuuchukua Msalaba pamoja na Yesu na kusonga mbele na safari ya maisha.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema, Yesu ametupa mfano. Ingawaje yeye anatoka kwa Mungu, " alikubali kushuka na kuikana nafasi yake, na akawa mtumishi kwa kila mmoja wetu.

Na huo ndiyo mtindo wa kutuokoa, alio waonyesha wafuasi wake, kwa ajili ya kuipatia furaha ya kweli, na kuwafanya wazae matunda bora . Ni njia ya kujikana na kuwa mtumishi kwa ajili ya wengine, ni njia inayodai kutenda kinyume na moyo wa ubinafsi na , uchoyo, moyo wa kudai yote yaliyo mema ni yangu peke yangu. Ni njia ya kujifunua wazi kwa ajili ya wengine , kwa sababu ni njia aliyoichagua Yesu, kuwa ndiyo mtindo unaofaa, na yeye hakusema tu lakini aliishi nakutembea katika njia hiyo , hadi kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kutukomboa sisi ili tupate stahili ya kuitwa wana wa Mungu . Na hivyo ni njia ya maisha ya unyenyekevu, sadaka na ukarimu.

“Kwa kuwa mtu anayetaka kuokoa maisha yake mwenyewe, lazima akubali kuyapoteza ," Yesu alifundisha na kutoa mfano wa mbegu ya ngano, kama isipozikwa aridhi na kufa, haiwezi kuzaa matunda. Hivyo mfano huu unatupatia maana ya kujitoa sadaka kwamba ni chanzo cha furaha , Papa alifafanua na kuongeza , kwa sababu ni yeye mwenyewe anayetupa furaha hii. Kumfuatia Yesu ni chanzo cha furaha , na ili kuipata furaha hiyo ni lazima kutembea ndani ya mtindo wa Yesu, si katika mitindo ya dunia. Kumfuata Yesu ina maana ya kuyatoa maisha kwa wengine . Ni kuwa na roho ya ukarimu. Ni kuukana ubinafsi wetu, unaotutaka tuonekane kuwa watu muhimu mbele ya wengine.

Papa Francisko ameeleza na kurejea mfano mzuri uliotajwa katika kitabu chenye jina” kumwigiza Kristo: Upendo usiotaka kujulikana na kuchukuliwa kama si kitu", akisema huo ndiyo unyenyekevu wa Kikristo, aina ya unyenyekevu na nafasi ya kwanza kwa Yesu. Na hii ni furaha yetu , na hii ni mafanikio ya yetu : kwenda pamoja na Yesu. Furaha nyingine zisizo zaa matunda bora, si Furaha, kama Yesu alivyosema , wanafikiria tu kuupata ulimwengu wote , lakini mwisho kuupoteza na kuharibifu maisha yao. Na hivyo tunapokianza kipindi cha Kwaresima na tumwombe Bwana, atufundishe mtindo wa maisha katika huduma ya Kikristo na furaha ya kujitolea sadaka kwa wengine na manufaa ya kutembea pamoja kama yeye mwenyewe alivyotaka.








All the contents on this site are copyrighted ©.