2014-03-06 09:45:33

Brazil kupambana na janga la biashara ya binadamu



(Vatican Radio) Baraza la Maaskofu Katoliki la Brazil ( CNBB ) Jumatano lilizindua Kipindi cha kwaresima 2014 na Kampeini inayolenga kaulimbiu ya mwaka huu "Udugu na biashara haramu ya binadamu.
Kauli mbiu iliyochaguliwa na Baraza , kutoka Waraka wa Mtume Paulo kwa Wagalatia (5,1) “Ni kwa uhuru kwamba Kristo ametuweka huru " .
Uzinduzi wa Kampeni hii ya 51 , uliongozwa na Katibu Mkuu wa Cnbb na Askofu Msaidizi wa Brasilia, Askofu Leonardo Ulrich Steiner, katika mkutano ulio hudhuriwa na wawakilishi wa Serikali, vyama vya kiraia na jumuiya za kidini.
Kampeni hii inalenga katika matazamio ya utendaji wa mipango mfululizo kwa lengo la kuelekea kuongeza uelewa wa , malezi na sala ili kuwawezesha uelewa mzuri wa matatizo ya biashara haramu ya binadamu na kuandaa " mawakala wa kichungaji" ambao watakuwa na uwezo wa kuijulisha kimyakimya jamii yenye nia ya kupambana dhidi ya biashara haramu ya binadamu
wa mujibu wa shirika la kujitegemea “Walk Free Foundation” linaeleza Brazil peke yake, kuna watu wasiopungua 200,000 wanaoishi katika hali za utumwa. Papa Francisko, akiwa amevutiwa na juhudi hizi za kukomesha mateso kwa binadamu alimtuma barua yake kwa washiriki wa uzinduzi wa Kampeni ya hii.
Papa katika ujumbe wake amewatia nguvu na kuonyesha mshikamano wake kwamba, katika kipindi hiki cha siku ya pili arobaini za Kwaresima , pia watakuwa pamoja nao kwa utambuzi zaidi kwamba Mungu alimtolea mwanae sadaka kwetu na pia kututaka sisi tujitolee sadaka kwa ajili ya wengine, hasa kwa wale wanaohitaji zaidi, kuwekwa huru. Kwa maana hii, Wakristu ni lazima kuhamasika na kuwa watu wa ukarimu katika jamii Brazil dhidi ya majanga ya kijamii ikiwemo biashara ya binadamu.
apa amewaombea ulinzi wa hali ya juu raia wote wa Brazil, ili waweze kuwa na maisha mapya katika Kristo, yenye kuwaweka huru wote kama watoto wa utukufu wa Mungu (Rm 8,21 ), kuamsha katika kila hisia za moyo wa upole na huruma kwa ndugu wengine, wake kwa waume , wanaohitaji kuwa huru.








All the contents on this site are copyrighted ©.