2014-03-05 11:11:49

Zaidi ya watu 900, 000 wamekimbia makazi yao Sudan ya Kusini


Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linasema kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea huko Sudan ya Kusini, watu zaidi ya laki tisa, wengi wao wakiwa ni watoto wamelazimika kuyakimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wa maisha yao. Vita inayoendelea Sudan ya Kusini inaweza kusababisha maafa makubwa kwa watoto nchini humo.

Ted Chaiban, Mkurugenzi wa UNICEF anayesimamia masuala ya dharura anasema, licha ya Serikali na Wapinzani kutia sahihi mkataba wa kusitisha vita, lakini bado mapigano yanaendelea na watu wanazidi kupoteza maisha. Zaidi ya watu 30, 000 wako hatarini kukosa makazi na hivyo kuhitaji msaada wa dharura kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa.

Inakadiriwa kwamba, kuna watu millioni 3. 7 wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa usalama wa chakula nchini Sudan ya Kusini. Jumuiya ya Kimataifa inawajibu wa kuwalinda na kuwasaidia raia na watoto wanaoendelea kuteseka kutokana na vita.







All the contents on this site are copyrighted ©.