Msalaba daima ni njia ya Mkristu : leo hii kuna wafia Ukristo wengi kuliko awali.
(Vatican Radio) Mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko , katika Ibada ya Misa ya mapema
asubuhi siku ya Jumanne katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta- Vatican, yalilenga
zaidi katika mateso ya Wakristo katika jamii ya kisasa. Aliwataka Wakristu kukumbuka
kwamba, Ukristu daima ni kuwa tayari kuubeba Msalaba, kama njia ya kumfuata Kristo.
Leo hii kuna Wakristo wengi wanaoifia imani yao kwa Kristo, kuliko wakati miaka ya
kwanza ya Kanisa.
Katika hotuba yake , Papa alirejea somo la Injili ambamo
Petro anamwuliza Yesu, nini wanafunzi wake, watapewa kwa kumfuata. Papa alieleza pengine
Petro alidhani kwamba kumfuata Yesu itakuwa shughuli kubwa ya kibiashara kwa sababu
Yesu ni mkarimu, lakini daima Yesu aliwaonya, malipo ya kumfuata, daima yataambatana
na mateso.
Papa Francisko aliendelea kuonya kwamba, Msalaba upo daima katika
njia ya ukristo! Na kwamba, kanisa litakuwa na waamini wengi katika jumuiya za Kikristo
na wengi wao watapambana na mateso. Hii ni kwa sababu dunia haivumilii utakatifu
wa Kristo. Haivumilii kusikia Neno la injili. Havumilii kuziishi Heri . Na hivyo
wale wanaomkiri Kristo wanapambana na mateso : kwa maneno, na vitendo , kama ilivyokuwa
kwa Wakristo wa karne ya kwanza , walishutumiwa vikali, kufungwa na kuuawa
Lakini
bahati mbaya binadamu husahau, Papa alieleza huku akifanya rejea kwa Wakristo wengi
wa miaka 60 iliyopita, waliodhulumika katika makambi ya kazi , katika makambi ya
jeshi dhalimu la Nazi, makambi ya Wakomunisti n.k. Na hivyo ndivyo hata leo hii...kuna
mashahid wengi zaidi wafia Ukristu , kuliko hata nyakati za karne ya kwanza ya Kanisa.
"
Papa Francis alisema kuwa kuna ndugu wengi na waume kwa wake , ambao
wanateseka kwa kumshuhudia Kristo katika maisha yao ya kila siku.. Baadhi hawawezi
kubeba Biblia mikononi mwao barabarani. Wanashutumiwa nakuwekwa hatiani kwa kosa
la kuwa Biblia . Hawawezi kuvaa msalaba . Papa anasema hii ndiyo njia ya Yesu. Lakini
ni barabara furaha kwa sababu Bwana wetu kamwe hatuweki katika majaribu yaliyo zaidi
ya uwezo wetu . Maisha ya Kikristu si kwa sababu za faida za kibiashara , wala si
ajira , lakini ni jambo jepesi la kuamua kumfuata Yesu. Na ndivyo inavyotokea katika
kumfuata Yesu.
Papa ameeleza na kuhimiza Wakristu kujenga ndani hamu ya
kuwa jasiri katika kumshuhudia Yesu, kwamba ni jambo jema leo hii kwa Wakristo wote
wake kwa waume. Papa aliangalisha mawazo yake kwa wale wasiokuwa na fursa ya kusali
pamoja, kwa sababu kufanya hivyo ni makosa , wale ambao hawawezi kuwa na kitabu cha
Injili au Biblia kwa sababu ni kosa kuwa na vitabu hivyo.
Papa alikamilisha
kwa kuwakumbuka pia wale ambao hawawezi kwenda Misa kwa sababu ni haramu nakutoa
mwaliko kwa Wakristo kujiuliza iwapo wako tayari kubeba msalaba na kuteseka, mateso
kama Yesu alivyofanya? Ni vizuri kwa kila mmoja wetu kwa kufikiri juu ya hili , alihitimisha.