Gustavo Andùjar Robles kutoka Cuba achaguliwa kuwa Rais wa SIGNIS duniani
Mkutano mkuu wa SIGNIS uliokuwa unafanyika mjini Roma kuanzia tarehe 25 Februari hadi
tarehe Mosi, Machi 2014 kwa kuwashirikisha wajumbe 300 kutoka katika nchi 80, wamemchagua
Gustavo Andùjar Robles kutoka Cuba kuwa ni Rais mpya wa SIGNIS, ambalo ni Shirikisho
la Wanahabari Wakatoliki Duniani. Wajumbe wamepata pia fursa ya kupitia Katiba Mpya
ya SIGNIS iliyopitishwa hivi karibuni na Baraza la Kipapa la Walei.
Rais Mpya
wa SIGNIS amewataka wajumbe kujifunga kibwebwe ili kuweza kukabiliana na changamoto
zinazoendelea kujitokeza katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na
teknolojia ya habari. SIGNIS inapaswa kuwa na mwelekeo mpana zaidi katika kukabiliana
na changamoto hizi.
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa maadhimisho
ya Mkutano mkuu wa SIGNIS mjini Roma, aliwataka Wanahabari Wakatoliki kusimama kidete
ili kupambana na changamoto za daima, ili waweze kutangaza hekima, ukweli na uzuri
unaofumbatwa katika Injili ya Kristo.
Viongozi wengine walioachaguliwa kuwa
Makamu wa Rais wa SIGNIS ni: Frank Frost kutoka Marekani. Lawrence John kutoka
Malaysia.