Ujumbe wa Papa Francisko kwa Maaskofu wa Hispania : dumuni katika utume wa Kanisa.
(Vatican) Papa Francis Jumatatu alikutana na Maaskofu Katoliki wa Hispania, wanapo
endelea na hija yao ya kitume ya ad Limina Visita , katika Idara za Vatican. Papa
akikutana nao kwa ujumla,hotuba yake, ililenga zaidi katika hali ya sasa ya Kanisa
nchini Hispania na dunia ya magharibi kwa ujumla.
Aliwaambia, kwa wakati
huu, wanapoteswa na ugumu wa wabatizwa wengi kutojali sheria na kanuni za kanisa,
ni lazima kutafuta mbinu za kukabiliana na utamaduni wa kidunia , unao shinikiza maisha
ya kidini kuwa ni maisha binafsi , na kutaka kumtoa Mungu katika mazingira ya umma.
Ni lazima watafute mbinu za pamoja kuonyesha jinsi ilivyo muhimu kwa mtu kutosahau
historia yake. Hivyo kutokana na hilo, wanapaswa kufundisha kwa ujasiri kwamba,
neema ya Mungu kamwe haiwezi kusitishwa na utendaji wa biandamu, na kwamba, fadhila
za Roho Mtakatifu zina endelea kufanya kazi hata katika hali halisi za sasa.
Baba
Mtakatifu aliwahimiza Maaskofu kuidhaminisha imani yao kwa Roho Mtakatifu, kupandikiza
mbegu ya imani thabiti katika mioyo yao wote, walio kabidhiwa katika huduma yao
ya kichungaji .
Papa alitia shime dugu zake katika Kristo na katika utumishi
wa Kanisa , kutoachia mwanya wowote kwenye jitihada za kufungua njia mpya kwa ajili
ya maisha ya Kiinjili, yaifikie mioyo ya watu wote , ili waweze kugundua kile ambacho
tayari kimehifadhiwa ndani ya Kristo kama rafiki na ndugu .
Aliwataka Maaskofu
hao kuyaweka Makanisa yao katika hali ya Utume wa Kudumu, kwa ajili ya kusaidia kuimarisha
imani , hasa kwa watoto, na kurejesha tena kanisani wale waliojitenga mbali na kanisa.
Papa alisema, imani si tu urithi wa utamaduni na mapokeo ya kijamii , lakini ni zawadi
inayotolewa kwa mtu anayekutana na Yesu na ni uhuru na furaha kamili katika kuyakubali
maisha mapya yaliyomo katika zawadi hiyo.
Papa pia aliita familia iliyo injilishwa
, kuwa wakala wa thamani katika kueneza Injili. Na hivyo aliwahimiza Maaskofu wa Hispania,
kuandaa vyema miito ya upadre. Na alimalizia hotuba yake kwa kusisitiza upendo
na huduma kwa maskini, kama ishara ya Ufalme wa Mungu , na Kanisa ni mama ambaye "
hawezi kusahau watoto wengi wanao ishi katika hali ya kupungukiwa na mahitaji msingi
ya binadamu