2014-03-04 15:12:11

Jibu la Kanisa kukabiliana na VVU/UKIMWI.


Vatican Radio) Umoja wa Mataifa na Chombo Katoliki kwa ajili ya misaada na ustawi wa jamii “Caritas Internationalis” , wiki iliyopita walikuwa wenyeji wa Mkutano wa Kimataifa ulio lenga kuimarisha ushirikiano katika kukomesha ambukizo la VVU na UKIMWI .

Mkutano wa siku mbili alio taja ufanisi wa mashirika ya kidini yanayo shiriki katika utoaji wa matibabu na huduma kwa watu wanaoishi na VVU. Pia uliotambua, uwepo wa changamoto kadhaa, ikiwemo , haja uwepo wa uwekezaji mkubwa ya fedha katika huduma za matibabu , na ushirikishwaji wa mashirika ya kidini katika kufanya maamuzi katika ngazi ya kitaifa.
Mmoja wa washiriki katika mkutano huo, Kardinali John Onaiyekan ya Abuja Nigeria, akizungumza na Mwana habari Lydia O'Kane kuhusu mwitikio wa Kanisa Katoliki VVU / UKIMWI katika ngazi ya chini mahalia, alieleza kwamba, kishindo cha athari za VVU hakiwezi kuacha kusikika katika ngazi za chini mahalia hadi hapo, mahubiri, mafundisho na Katekesi za kanisa, vitakapo fanywa kuwa sehemu ya maisha ya watu mahalia.

Kardinali aliendelea kueleza kwamba, ni jukumu la Paroko na Mapadre wenzake ambao wamepata mafunzo seminarini, ya kuwa viongozi wa kanisa, na kuwa sauti ya Kanisa na watu katika ngazi za chini.
Mkutano huo ,ulioandaliwa kwa pamoja na UNAIDS na Caritas Internationalis , ulikamilika Februari 26 na wito kwa makundi ya kidini kuwa na jitihada za kipekee kwa ajili ya walioathirika na ugonjwa wa UKIMWI na hata wale wanaowasaidia.
Daktari Brazil Luiz Loures ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na Naibu Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, akishiriki katika mkutano huu alieleza kuwa ,si rahisi kutokomeza janga la Ukimwi, kutokana na maendeleo yaliyopo sasa dhidi ya ugonjwa , bila ya kuyashirikisha zaidi mashirika ya kidini na hasa mashirika ya Katoliki, ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kutokomeza virus vya UKIMWI. .

Alieleza hilo kwa kutoa ushahidi unaonyesha kwamba, asilimia 96% ya watu waliotibiwa virusi , wana uwezekano wa kueneza virusi hivyo kwa wapenzi wao wa karibu au wake au waume zao, na hivyo idadi ya wenye virusi haitakuwa zero, lakini taratibu idadi itaendelea kupungua kutokana na uwepo wa tiba na hivyo kunakuwa na tumaini la ugonjwa huu kutokuwa tena tishio la kimataifa kama ilivyo kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 30 iliyopita ...

Na kwamba wanalenga kutoa matibabu kwa watu milioni 15 ifikapo mwaka 2015 .... kushinikiza watu kupata tiba mapema iwezekanavyo ..... na ni matumaini yao kwamba, mashirika ya kidini yatakuwa mstari wa mbele kujihusisha na kuongeza jitihada za kuelimisha watu juu ya hili. .

Na kwamba bado kuna unyanyapaaji na ubaguzi mwingi kwa wenye virusi, Na ndiyo maana wanahitaji taasisi na mashirika kama Kanisa na misikiti kuzungumzia dhidi ya ubaguzi huu. Kwa kufanya hivyo, ni wazi kwamba, wataweza kutoa msaada zaidi kwa watu kuamua kupimwa na kupata matibabu haraka iwezekanavyo ...








All the contents on this site are copyrighted ©.