2014-03-04 08:58:43

Burundi na Vatican zimeridhia mahusiano msingi


Ijumaa iliyopita 28 Februari 2014, katika Makao makuu ya Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Jamhuri ya Burundi, Waziri Laurenti Kavakure , na Askofu MkuuFranco Coppola , Askofu Mkuu wa jina wa Vinda ambaye ni Mwakilishi wa Papa nchini Burundi, kwa uwezo waliodhaminishwa , walibadilishana hati za makubaliano kwa ajili ya kutendea kazi, maridhiano yaliyofikiwa kati ya Jimbo Takatifu na Jamhuri ya Burundi, kwa ajili ya maslahi ya pamoja , iliyosainiwa Bujumbura tarehe 6 Novemba 2012.

Maridhiano hayo yenye kutambua maendeleo mazuri katika uhusiano kati Jimbo Takatifu na Jamhuri ya Burundi, kwa kipindi cha zaidi ya miaka hamsini, unatoa ufafanuzi na hakikisho la dhamana ya hadhi ya kisheria ya Kanisa Katoliki na kanuni zake, kwenye vipengere mbalimbali vya kisheria, kama ndoa, maeneo ya ibada , taasisi Katoliki za elimu na mafunzo, ustawi na hisani ya Kanisa , huduma za kichungaji katika majeshi ya ulinzi na mazingira ya magereza , hospitali , na haki ya kanisa katika urithi wa mali zake na malipo kodi kisheria.

Hati ya Mkataba huu msingi , ambayo ina Utangulizi na vipengere 22 vya maelezo yaliyoambatishwa, imepitishwa na kuwa chombo cha kufanyia kazi maridhiano kwa mujibu wa sheria Ibara ya 22. 1 .
Kitendo hiki cha kubadilishana hati kilishuhudiwa :
Kwa niaba ya Jimbo Takatifu, Askofu Gervais Banshimiyubusa wa Jimbo la Ngozi, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Burundi ( CECAB ); Askofu Mkuu Evariste Ngoyagoye Jimbo Kuu la Bujumbura, makamu wa rais wa CECAB ; Askofu Joaquim Ntahondereye wa Jimbo la Muyinga ; Askofu Bonaventure Nahimana wa Jimbo la Rutana ; Askofu mteule Georges Bizimana, Mwenye haki ya kurithi Jimbo la Bubanza ,Padre Josè Nahumu Jairo Salas Castaneda Mtendaji katika Ofisi ya Kitume ya uwakilishi wa Papa Burundi, na Padre A. Lambert Niciteretse , katibu mkuu wa CECAB. ;
Kwa niaba ya Jamhuri ya Burundi , Emile Butoyi ,Mkuu wa itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ; Balozi Egyde Ndikuriyo ,Mkurugenzi Mkuu kwa Ulaya, Marekani na mashirika yasiyo ya kiserikali ; Balozi Antoine Ntahobwa ,Mkurugenzi kwa ajili ya Amerika, Balozi Ernest Ndabashintze , Mshauri wa waziri wa Mambo ya Nje; na Emerence Nahonkuriye ,Naibu Waziri i wa Mambo ya Nje.








All the contents on this site are copyrighted ©.