2014-03-03 16:01:28

Watu wa leo wake kwa waume, wanahitaji kukutana na Mungu- Papa


Mapema Jumatatu hii Papa Francisko alikutana na washiriki wa Mkutano wa FIES ambao wamejumuika kwa lengo la maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya kuanzishwa Shirikisho la Mazoezi ya Kiroho, ambalo huwajibika na kazi ya uhamasishaji na msaada kwa ajili ya mazoezi ya kiroho, hata Italia. Papa kupitia kwa Askofu Mkuu John Scavino, kwa moyo wa kibaba alitoa salaam zake za upendo kwa wote wanao husika na Shirikisho hili.


Papa ameyataja maadhimisho ya miaka mwaka huu kuwa ni fursa nzuri kwa ajili ya kupima vyema yaliyopita na wanakoelekea kwa kusoma ishara mpya za nyakati mara kwa mara. Kwa hiyo, ni muhimu kukumbuka lengo la Shirikisho , ambayo ni " kuongeza uelewa wa mazoezi ya kiroho , lengo kama uzoefu na nguvu ya Mungu katika hali ya hewa ya kusikiliza Neno, inakuwa ni uongofu na kujitolea ya dhati katika utendaji wa binafsi kwa Kristo na Kanisa zima.


Papa aliendelea kusema, mandhari walioichagua kwa ajili ya maadhimisho haya , Upendo katika uzuri wa kiroho kwa ajili ya kueneza harufu ya Kristo" (cf. 2Kor 2:14), inaonyesha imani kwamba, pendekezo la Mazoezi ya Kiroho linalotolewa ni wito unaokaribisha uzoefu kukaa na Mungu kwa upendo wake wa uzuri wake. Ambaye anauishi ukweli huu wa kuwa na mazoea ya kuwa karibu na Mungu daima, unakuwakuwa ni uzoefu wa kuvutia, kuburudisha na kufanya upya sura ya maisha ya kawaida, daima kueneza harufu nzuri ya Kristo.
“Wanaume na wanawake wa leo hii, wana haja ya kumtafuta Mungu , kumjua na si kuwa na tetesi (soma Ayubu 42.5 ). Huduma yenu leo hii, na malengo yenu ni lazima kufanya hivyo. Kutoa nafasi ya kusoma Neno la Mungu katika ukimya na sala. Mazingira pekee yanayopatikana kwa ajili ya uzoefu huu wa kiroho, huwa ni ni makazi ya kiroho, ambayo huendelea kukua katika mtazamo wa kudumisha na kuunda mtu mpya kiroho”.
Papa amewahimiza wachungaji katika jumuiya mbalimbali, kujishughulisha kazi hii, ili kusikosekane nyumba za mazoezi ya kiroho, wakiwepo pia wahudumu waliofundwa vyema na wahubiri walioandaliwa vizuri, waweze kutoa mafundisho bora ya kiroho, yenye kuonyesha kweli nguvu ya Roho Mtakatifu, ambaye huungana nasi na kutudumisha katika maombi na sala
Papa alimalizia hotuba yake, kwa wanachama wote wa shirikisho hili la kiroho kuendelea kutoa mchango na msaada wao katika mazoezi ya Kiroho na kufanywa upya kama dhamana yao ya kushikamana na Yesu daima. Papa aliomba ili kwamba Roho Mtakatifu, awasaidie kuzingatia masharti ya Kristo, na pia msaada wa inasaidia kuelewa kwamba maombi ni njia ya lazima ya muungano pamoja naye katika njia ya msalaba hadi kusulubiwa. Sala ni njia inayotufikisha katika umoja na Yeye aliyesulubiwa.
Papa alikamilisha akisema , Asante kwa huduma hii muhimu, mnaoitoa nyinyi katika Kanisa, Enezeni zoezi ili tunu za Injili ziweze kuwafikia wote. Aliomba msaada wa Mama Yetu Maria, daima uwatangulie katika kazi hii. Pia aliwataka wasimsahau katika sala zao na Papa aliahidi kuwakumbuka k atika sala zake na kuombea ingi wa baraka za mbinguni”.









All the contents on this site are copyrighted ©.