Baba Mtakatifu Francisko, amehimiza Wakristu, waongeze bidii kuombea miito ili wapatikane
makuhani na watawa walio iva kweli kiroho kwa ajili ya kumtumikia Bwana peke yake.
Watumishi walio jinasua kweli kutoka ubatili wa ibada za sanamu na mamlaka na fedha
. Papa alitoa himizo hilo wakati wa Ibada ya Misa, Jumatatu hii asubuhi , akiwa katika
kanisa dogo la Mtakatifu Marta.
Hotuba ya Papa ililenga katika Injili ya Siku,
ambamo mtu tajiri anapiga magoti mbele ya Yesu na kuuliza nifanye nini ili niweze
kuupata uzima wa milele. Papa alisema, . Mtu huyu alikuwa na hamu kubwa ya kusikia
maneno ya Yesu. Inaonyesha alikuwa mtu mwema, kwa sababu tangu ujana wake alikuwa
ametii amri. Pamoja na utajiri wake, aliona bado kuna kitu anachokihitaji , Roho Mtakatifu,
alimwongoza kwa Yesu, kutaja kujua zaidi cha . Yesu alimwangalia kwa upendo na kumwambia
, nenda kauze vyote ulivyo navyo na njoo ufuatane nami katika kuitangaza Injili. Lakini
hiyo , aliposikia hayo, alishikwa huzuni moyoni mwake kuachana na mali yake haikuwa
rahisi.
Papa alisema, “Moyo wa tajiri, ulihangaika ,kwa sababu Roho Mtakatifu
alikuwa akimtaka awe karibu na Yesu na kumfuata,nae alikuwa na moyo kamili lakini
ulioinamia mali, na akuwa na ujasiri wa kuviacha alivyo navyo. Hivyo akachagua fedha
. Moyo uliojaa matamanio ya fedha ...ingawa hakuwa mwizi, laghai, wala mwenye kuvunja
sheria na makosa mengine ya jinai. Alikuwa mtu mwema na mwaminifu. Lakini moyo wake
alifungwa na mapenzi kwa mali, alikuwa amefungamana na fedha na hivyo hawakuwa na
uhuru wa kuchagua. Alichagua fedha kuwa msingi wa maisha yake”.
Papa alieleza
na kurejea kwa jinsi gani vijana wengi , husikia ndani ya mioyo yao wito kama huu
wa kuwa karibu na Yesu wakiwa wamehamasika na bila ya aibu hupiga magoti mbele ya
Yesu na kuonyesha hadarani imani yao katika Yesu Kristo na wakiwa wanaonyesha moyo
wa kupenda kumfuata yeye , lakini kumbe ndani ya mioyo yao pia wamejaa matamanio mengine
mengi yanayowapokonya ujasiri wa kumfuata , na hurudi nyuma , furaha hayo ikiishia
kuwa huzuni kubwa.
Kwa ajili ya hili, Papa amehimiza maombi k wa ajili ya
vijana hawa ili mioyo yao ijae tu mapenzi kwa Yesu na kuwa tupu kwa mambo mengine.
Kuwa na maombi kwa ajili ya miito,. Tusali ili Bwana, aweza kuwa na watumishi wengi
wa kutuma katika shamba lake. Kutuma Mapadre, kutuma , kutuma watawa ,kutuma makuhani
kwa ajili ya kuzuia ibada za sanamu, ibada ya sanamu ya ubatili , ibada ya sanamu
ya kiburi , ibada ya sanamu ya mabavu, ibada ya sanamu ya fedha . Ni lazima tuombe
kwa ajili ya kuandaa mioyo ya kumfuata Yesu kwa karibu.
Papa alisema mtu huyu
katika Injili , alikuwa ni mtu mzuri mno lakini alikosa ujasiri wa kuachana na mambo
ya duni aili aipate furaha ya uzima wa milelle. Leo hii kuna vijana wa namna hiyo,
tunaohitaji kuwaombea ili wajinasue na utajiri wa dunia na mambo yake, badala yake
washibishwe na utajiri wa kuwa karibu na Yesu na kumfuata.