2014-03-03 12:24:48

Maendeleo ya Wananchi wa Guinea Bissau hayana budi kupewa kipaumbele cha kwanza


Umoja wa Mataifa umeitaka Serikali ya Guinea Bissau kuhakikisha kwamba, inatoa kipaumbele cha kwanza kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii, ili wananchi wote wa Guinea Bissau waweze kuwa na matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi. Ili kufikia lengo hili kuna haja ya kuwa na mwono mpana, sera na mbinu mkakati wa kuweza kuwajengea wananchi matumaini mapya.

Hayo yamesemwa hivi karibuni naMadgalena Sepulveda, Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki msingi za binadamu. Serikali haina budi kuboresha utawala wa sheria pamoja na kuweka mikakati thabiti ya kupambana na umaskini wa hali na kipato, unaoepelekea uvunjaji wa haki msingi za binadamu. Serikali iwekeze katika huduma za kijamii pamoja na kuimarisha sekta ya kilimo, ili kuweza kuwa na uhakika wa usalama wa chakula pamoja na kuboresha kipato cha familia nyingi za watu wanaoishi vijijini.







All the contents on this site are copyrighted ©.